Aprili 21, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, imemtia hatiani Mshtakiwa Bw. PONSIAN MUBAYOBA katika Shauri la Uhujumu Uchumi Na.02/2022, lililokuwa mbele ya Mhe. Daniel Nyamkerya na likiendeshwa na Mwendesha Mashtaka William Fussi.
Katika shauri hilo, mshtakiwa alikua anashtakiwa kwa makosa matatu, mawili yakiwa ya matumizi ya nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri k/f 22 PCCA na la mwisho ni Ubadhirifu wa kiasi cha sh. 1,000,000 k/f 28(1) cha PCCA.
Mshtakiwa alikiri mashtaka yote kwamba ni kweli alitenda makosa hayo huku akijua kabisa ni kinyume na sheria.
Baada ya kukiri mshtakiwa alitiwa hatiani kwa kufanya makosa hayo na katika kuomba shufaaa waliomba kupewa adhabu ndogo kwani ni wakosaji wa mara ya kwanza na ana familia inayomtegemea.
Upande wa mashtaka uliiomba mahakama kutoa adhabu kwa mujibu wa sheria.
Mhe. Hakimu Mkazi baada ya kuzingatia hoja za pande zote mbili alimpa adhabu ya fine ya shilingi za kitanzania laki tano (sh. 500,000) kwa kosa la kwanza la matumizi ya nyaraka au kifungo cha miaka 3.
Adhabu ya fine ya shilingi za kitanzania laki tano ( sh. 500,000) kwa kosa la pili la matumizi ya nyaraka au kifungo cha miaka 2.
Na fine ya sh. 400,000 kwa kosa la ubadhirifu wa sh. 1,000,000 au kifungo cha mwaka mmoja.
Aidha Mhe Hakimu alitoa amri ya kiasi sh. 1,000,000 kilichofanyiwa ubafhirifu kirudishwe katika mamlaka husika. TAKUKURU Muleba Aprili 21, 2023