Januari 19, 2023 imefunguliwa Kesi ya Jinai namba 136/2023 katika Mahakama ya Wilaya Ilala, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala Mhe. Suzanne Kihawa.
Washitakiwa ni Bw. Ramesh Naranbhai Patel, ambaye alikua Mkurugenzi na Mjumbe wa Bodi wa iliyokua Bank M na mshtakiwa wa pili ni Bw. Richard Mwera Nicholaus Matiku ambaye ni mjasiriamali.
Kesi hiyo inaendeshwa na Waendesha Mashtaka wa TAKUKURU, IMANI NITUME akisaidiwa na Mwanasheria VERONICA CHIMWANDA.
Washtakiwa walisomewa hati ya mashtaka ya kughushi saini katika nyaraka mbalimbali za Bank M ili waweze kujipatia mkopo wa shs. 920 millioni .
Makosa haya yanadaiwa kutendeka wakati mshtakiwa wa kwanza alipokuwa Mjumbe wa Bodi ya Bank M.
Washtakiwa wamekana mashtaka na wametolewa nje kwa dhamana baada ya kukidhi masharti na vigezo vya dhamana.
Kesi imeahirishwa hadi May 18, 2023 kwa ajili ya kusoma hoja za awali.