Katika Mahakama ya Wilaya ya Missenyi mnamo Aprili 20, 2023, limefunguliwa Shauri la Jinai Na.02/2023 mbele ya Mhe. Muyombo
Katika shauri hilo washtakiwa wawili Bw. James Damian Kimario na Jacob John Ngowi walishtakiwa na Jamhuri kwa kosa la kujihusisha na vitendo vya Rushwa chini ya kifungu cha 15 (1) (b) & (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa SURA ya 329 marekebisho ya Mwaka 2022 kwa kutoa fedha ya hongo shilingi Milioni 10 (sh 10,000,000/=).
Fedha hizo zilitolewa kwa Maafisa wa Serikali wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ili waweze kuachiwa baada ya kushikwa na bidhaa za magendo.
Waliposomewa mashtaka yao na Waendesha Mashtaka wa TAKUKURU, walikiri makosa yao
na kutiwa hatiani kwa kufanya kosa hilo chini ya kifungu cha 15 (1)(b) & (2) cha PCCA na kupewa adhabu ya kulipa faini ya shilingi laki tano (sh. 500,000) kila mmoja au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela .
Aidha Mahakama ilitoa amri ya kutaifishwa kwa shilingi milioni kumi kuwa mali ya Serikali na kuelekezwa kuwa fedha hizo ziwekwe katika akaunti ya TAKUKURU.
TAKUKURU Missenyi, Aprili 20, 2023