Kesi namba ECC 4/2023 imefunguliwa Aprili 19, 2023 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni iliyopo Kinondoni.
Mshitakiwa ni Bw. Shadrack Mayala– aliyekuwa Mwalimu Chuo cha Paradigms College of Health Sciences ltd
Ameshitakiwa kwa kosa la Rushwa ya Ngono kinyume na Kifungu cha 25 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa SURA ya 329, ikisomwa pamoja na Aya ya 21 ya Jedwali la kwanza na Kif cha 57(1) na 60(2) ya Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura 200 rejeo ya 2002.
Amesomewa shtaka lake mbele ya Hakimu Mkazi Mahakama ya Kivukoni iliyopo Kinondoni Mhe. Mushi.
Kesi imeahirishwa hadi Mei 22, 2023 itakapokuja kwa ajili ya kusikilizwa hoja za awali(PH).
Mshtakiwa yupo nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana .