APRILI 19, 2023, katika Mahakama (W) Kibiti mkoani Pwani, chini ya Mhe. Kisoka, limefungua Shauri No ECC / 04/2023 la Uhujumu Uchumi chini ya Sheria ya Kudhibiti Utakatishaji wa Fedha Haramu ya Mwaka 2022 pamoja na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa SURA ya 329, dhidi ya Geofrey William Haule na wenzake nane.
Washtakiwa wameshtakiwa kwa makosa ya kuomba hongo ya sh 10,000,000/= na kupokea hongo ya sh 2,990,000/=
ambazo aliweza kuzitakatisha.
Washtakiwa wawili, makosa yao hayana dhamana hivyo wamepelekwa mahabusu na wengine wako nje kwa dhamana.
Kesi itakuja tarehe 04.05.2023 kwa hoja za awali.