Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi. Neema Mwakalyelye amepokea kitabu kilichoandikwa na Binti Precious Fredrick mwenye umri wa miaka 13 kinachoitwa NILINDE. Ndani ya kitabu hiki, pamoja na mambo mengine binti huyo anayesoma Kidato cha Kwanza katika shule ya ‘Little Sisters of ST. FRANCIS – Simiyu, ameandika kuhusu namna rushwa inavyomnyima mtoto haki zake. TAKUKURU MAKAO MAKUU Aprili 18, 2023