KUTOKA MAHAKAMANI TABORA

Kesi namba ECC 4/2023 imefunguliwa Aprili 17, 2023 katika Mahakama ya Wilaya Tabora mkoani Tabora.

Mshitakiwa ni Bw. Leonard Wilson Chishomi– Mhasibu Chuo cha Nyuki Tabora

Anashitakiwa kwa makosa tisa ya kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri kinyume na Kifungu. Cha 22 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa SURA ya 329, ikisomwa pamoja na Aya ya 21 ya Jedwali la kwanza na Kif cha 57(1) na 60(2) ya Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura 200 rejeo ya 2002.

Ubadhirifu na Ufujaji wa Mali ya Umma kinyume na Kif. 28 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329 pamoja na Kugushi nyaraka kinyume na Kif. cha 333, 335(d)(I) na 337 vya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 rejeo ya 2019 na kujipatia kiasi cha sh. 6,430,000

Amesomewa mashtaka mbele ya Hakimu wa Wilaya Tabora Mhe. D.S .Nyakunga

Kesi imeahirishwa hadi Aprili 20 2023 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Mshtakiwa alikosa dhamana na kupelekwa gerezani.

Taarifa kwa Umma

KUTOKA MAHAKAMA YA WILAYA – MBOGWE, GEITA