Wakiwa na nyuso zilizojaa furaha ni watumishi wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu baada ya kutembelewa na Mkurugenzi Mkuu CP. Salum Rashid Hamduni ambapo ziara hiyo imeamsha ari mpya ya utendaji kwa watumishi hao. Mkurugenzi Mkuu amewapongeza watumishi hao kwa utendaji mzuri na kuwataka kuongeza jitihada zaidi ili kukidhi matarajio ya wananchi na Taifa kwa ujumla katika kutokomeza vitendo vya Rushwa. TAKUKURU Simiyu. Aprili 13, 2023.