Kesi namba CC 41/2023 imefunguliwa Aprili 13, 2023 katika Mahakama ya Wilaya Kibiti mkoani Pwani. Mshitakiwa ni MAGRETUS SIMON KAPENDAROHO – Mwenyekiti Kitongoji cha Songa – Mchukwi.
Anashitakiwa kwa kosa la rushwa chini ya kifungu cha 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa SURA ya 329.
Amesomewa mashtaka saba ya kuomba na kupokea rushwa ya sh 140,000 kutoka kwa wafanyabiashara wa Pombe Haramu ili asiwachukulie hatua za kisheria, mbele ya Hakimu wa Wilaya Mhe. Kisonga.
Kesi imeahirishwa hadi Aprili 27, 2023 itakapokuja kwa PH.
Mshtakiwa yuko nje kwa dhamana.