APRILI 12, 2023, katika Kesi Namba ECO 9/2022, Mshitakiwa Beaty Alex Kimaro ametiwa hatiani na Mahakama ya Wilaya ya Rombo kwa kutenda kosa chini ya kifungu cha 28 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329.
Mshitakiwa huyo ambaye aliajiriwa na Halmashauri ya Wilaya ya Rombo kwa nafasi ya mkusanya ushuru kwa njia ya POS, alikusanya kiasi cha sh. 1,985,000 bila kuwasilisha kwa mwajiri wake.
Mshitakiwa ameamriwa kwenda jela ama kulipa faini na ametakiwa kurejesha kiasi chote cha fedha alizokusanya na kushindwa kuwasilisha kwa mwajiri wake.