Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni, amefanya Kikao Kazi na Watumishi wa TAKUKURU Mkoa wa Mara na kuwataka kutekeleza majukumu kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa TAKUKURU wa Mwaka 2022/23 – 2025/26. Amewataka watumishi kuboresha utendaji kazi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea huku wakizingatia maadili ya TAKUKURU na ya Utumishi wa Umma ikiwa ni pamoja na kutojihusisha na uvujishaji wa siri. TAKUKURU MARA, Aprili 13, 2023.