Aprili 6, 2023, TAKUKURU Temeke imemkamata Kaimu Afisa Miliki Mkuu (Estate Manager) wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ofisi ya ILALA, kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni tatu (Sh.3 000,000/=).
Fedha hizo aliziomba na kuzipokea toka kwa Mtanzania mwenye asili ya Kiasia ili asitishe notisi ya kukatisha mkataba wa upangaji sehemu ya Biashara.
Inadaiwa kuwa Notisi hiyo alimpa Mtanzania huyo kwa madai kuwa ameshindwa kuzingatia masharti ya upangaji.
Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya sikukuu.