Aprili 6, 2023, Shauri la Jinai Na 69.2023 dhidi ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Same Mhe. David George Abel, limefunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Same.
Mshtakiwa amesomewa jumla ya makosa mawili ya kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15 (1)( a)( b) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa SURA ya 329.
Mshtakiwa amekana mashtaka yote na yupo nje kwa dhamana.
Shauri hilo litakuja tena kwa kutajwa Aprili 21, 2023.