Aprili 5, 2023, Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi imemtia hatiani aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa anakabiliwa na Kesi ya Uhujumu Uchumi Na 2.2021 na kumpatia adhabu ya kutumikia kifungo cha nje kwa mwaka mmoja na kumlipa mlalamikaji Bw. Alex Elibariki Swai kiasi cha shs 5,000,000 .
Aidha hukumu hiyo imetolewa baada ya mshtakiwa kukiri makosa kufuatia ‘plea bargaining’ iliyofanyika baada ya mshtakiwa kuomba kufanya maridhiano ambayo yalipewa baraka na ofisi ya DPP .
Aidha kiasi cha sh mil 5 kilikubaliwa na mlalamikaji baada ya mshitakiwa kumuomba kwamba hana fedha kwa sasa ila anakubali alimtendea vibaya na kweli aliomba na kupokea fedha zake jumla ya sh. 50,000,000/= na kumuomba amsamehe.