Machi 31, 2023, TAKUKURU Mkoa wa Katavi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Mpanda, imefungua kesi ya Jinai Na. CC. 26/2023 dhidi ya ROSE ELIAS MICHAEL (Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mbugani, Kata ya Kakese, Wilaya ya Mpanda).
Rose ameshtakiwa kwa makosa ya kuomba rushwa ya shs. 45,000/= na kupokea rushwa ya shs. 40,000/= kutoka kwa mwananchi aitwaye Manyeru Njigirwa Jitara (Mzazi wa Mwanafunzi), ili asimchukulie hatua kutokana na mtoto wa Mzazi huyo, aliyekataa kwenda shule ya sekondari.
Kesi hiyo imesikilizwa na Hakimu Mkazi Mheshimiwa LUOGA, ambapo mshitakiwa amekiri makosa yote mawili na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita (6) jela au kulipa fine ya shs. 100,000/=