KUTOKA MAHAKAMA YA WILAYA MOSHI, KILIMANJARO.

Machi 31, 2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Moshi, Shauri la Uhujumu Uchumi namba 30/2021 lililokuwa mbele ya Mhe. NAOMI MWIRINDE, likiendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, WAKILI FURAHINI KIBANGA, limetolewa hukumu ambapo Mshtakiwa JULIUS WILLIAM KIMARO
ametiwa hatiani kwa kosa la Matumizi Mabaya ya Mamlaka kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa SURA ya 329.

Awali alishtakiwa kwa matumzi ya kiasi cha sh. 600,000 kwa safari hewa ya kikazi na kuamriwa kulipa faini ya shs. 500,000/= au kwenda jela miaka miwili.