KUTOKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI, TANGA.

Machi 31, 2023 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga, kwenye Shauri la Uhujumu Uchumi namba 09/2021 lililokuwa likiendeshwa na Mawakili wa Serikali Anitha Kuringe, Khadija Luwongo na Joseph Mulebya, mbele ya Mhe. Aloyce Masua, imetolewa hukumu na Jamhuri imepata ushindi ambapo Mshtakiwa Mohamed Ally Jaka
ametiwa hatiani kwa kosa la Ubadhilifu kinyume na kifungu cha 28 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa SURA ya 329 marejesho ya Mwaka 2022.

Awali Mshitakiwa alifikishwa Mahakamani hapo alishtakiwa kwa kufanya ubadhilifu kwa kutowasilisha fedha kiasi cha Sh.4,528,000/= ambazo ni Mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, alizokusanya kupitia Mfumo wa POS.

Mshtakiwa amehukumiwa kulipa faini ya Shilingi Milioni Mbili au kwenda Jela kutumikia kufungo Cha miaka 2.

Mshtakiwa pia ameamriwa kurejesha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mkinga, fedha alizofanya ubadhilifu ambayo ni Sh.4,528,000/=.

Taarifa kwa Umma

NUKUU