Machi 21, 2023, Wakili katika Mji wa Geita, Bw. Otmary Gerald Komba, alitiwa hatiani na Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita na kuhukumiwa kulipa faini ya sh. 1,000,000/= au kutumikia kifungo jela cha muda wa mwaka mmoja.
Pamoja na hukumu hiyo, mahakama hiyo ilimwamuru Wakili huyo kurejesha fedha kwa mteja wake kiasi cha sh. 29,000,000/=.
Hayo yalitokea baada ya Wakili Komba kushtakiwa katika Mahakama hiyo chini ya kifungu cha 302 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu SURA YA 16, iliyo rejewa Mwaka 2022.
Chini ya kifungu hicho, Wakili Komba alikabiliwa na mashtaka katika Shauri Na. 291/2021, ambapo alijipatia fedha kutoka kwa mteja wake kwa njia ya udanganyifu.
Shauri hilo lilikuwa mbele ya Mhe. Wane na kusimamiwa Mahakamani kwa upande wa Jamuhuri na Mawakili wa Serikali Antidius Rutayuga na Ruth Ndetto.