Machi 29, 2023 katika Mahakama ya Wilaya Nachingwea, imefunguliwa Kesi ya Jinai Na. 35/2023 dhidi ya Mshitakiwa Rashid Ally Muheka, Mwenye Miaka 48, Mwenyekiti wa NAKAHIMBA AMCOS, iliyopo Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.
Mshtakiwa ameshtakiwa kwa kosa la kutoa hongo Kinyume na Kifungu cha 15 (1) (b) na 2 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Cap 329 R.E 2019).
Hongo hiyo ilikua ya jumla ya sh. 700,000/= iliyotolewa kwenda kwa Freita Kwayu – Mkulima wa korosho, ili kumshawishi asiweze kwenda ofisi za TAKUKURU Wilaya ya Nachingwea, kufuatilia suala la wizi wa korosho alizopeleka kwenye AMCOS hiyo.
Mshitakiwa alikiri kosa hilo na kupigwa faini ya sh 500,000/= au kutumikia kifungo cha miaka 3 jela.