Machi 28, 2023, limefunguliwa shauri la jinai namba 20/2023, JAMHURI Dhidi ya MAMBE MOHAMED MAMBE, ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Nasetani, Kata ya Engusero mkoani Manyara.
Shauri hilo linahusu kosa la kuomba na kupokea Rushwa ya shilingi 70,000 kutoka kwa mwananchi wa Kijiji cha Nasetani ili asichukuliwe hatua kwa kosa la kuendesha mkutano na wafugaji bila idhini ya uongozi wa Kijiji.
Mshitakiwa amekana makosa yote mawili yanayomkabili, lakini yupo ndani (rumande) baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyowekwa na Mahakama.