Ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Ilala imefanikiwa kufungua kesi moja kwenye Mahakama ya (W) Ilala Kesi Na. 96/2023.
Mshitakiwa: BAKARI HERIEL MCHOME Mtendaji wa Mtaa Pugu-Kinyamwezi.
Kosa ni kuomba hongo ya sh. 1,000,000/- na kupokea Tshs. 1,000,000/- kama kishawishi ili aweze kumpatia Mlalamikaji orodha ya watu waliovamia shamba lake kinyume na K/f cha 15(1)(a) na (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329 Rejeo la 2022.
Mshitakiwa amekosa dhamana kwasababu hakuwa na wadhamini.
Shauri hili limepangwa kwa usikilizwaji wa awali Tar. 6/4/2023