KUTOKA MAHAKAMANI TABORA

Machi 27, 2023, imefunguliwa kesi
CC No. 21/2023 katika Mahakama ya Wilaya Tabora.

HOSEA CHRISTOPHER NJILOE, ameshitakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea hongo kutoka kwa wananchi walioomba ajira YAPI MERKEZI Railway Construction Company.

Mshtakiwa amekiri kosa na kuhukumiwa kulipa faini sh. 500,000/=.

Katika hatua nyingine ilifunguliwa kesi
CC. No 22/2023 Mahama ya Wilaya Tabora mbele ya Mh. Sigwa Mzige.

Washtakiwa MWALIMU JUMA KAUDUNDE, JESICA JOHN JONATHAN na DANIEL JULIUS MASSAGA, wameshitakiwa kwa kuomba na na kupokea hongo ya 500,000/= kwa nia ya kusaidia kutoa ajira.

Washtakiwa wamekiri makosa na kuhukumiwa kulipa faini sh. 500,000/= kila mmoja.

Hadi tunatoka Mahakamani Mshtakiwa Mwalimu Juma Kaudunde alikuwa hajalipa faini na kupelekwa gerezani.

Taarifa kwa Umma

MWANASHERIA WA HALMASHAURI YA WILAYA MAKETE MBARONI KWA TUHUMA YA RUSHWA