Machi 28, 2023 katika Mahakama ya Wilaya Mbarali, limefunguliwa Shauri la Uhujumu Uchumi Na. 09/2023 dhidi ya Bw. Athumani Mwasomba ambaye alikiwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Rujewa iliyopo Halmashauri ya (W) Mbarali.
Mshtakiwa anashtakiwa kwa kosa la Kuisababishia hasara Halmashauri ya (W) Mbarali kiasi cha shs. 44,000,000/=.
Shauri limepangwa kuendelea kwa hatua ya kuanza kusikilizwa Maelezo ya Awali (Phg) Machi 29, 2023