Machi 24, 2023, Mhand. Joseph Mwaiswelo, Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma TAKUKURU (aliyeketi kiti cha mbele), kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, amepokea ugeni wa Viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi – Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), waliofika kwa lengo la kujifunza, kuimarisha mahusiano pamoja na ushirikiano.
Akizungumza na viongozi hao walioongozwa na Bw. Fred Romanus Sanga – Katibu Mkuu Mtendaji wa TAHLISO (Kulia kwa DCE), DCE amewapongeza TAHLISO kwa kuweka ajenda za Rushwa pamoja na Madawa ya Kulevya kama moja ya maeneo muhimu katika uendeshaji wa TAHLISO. Pamoja na mazungumzo, Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma aliwasilisha mada iliyolenga kuwawezesha viongozi hao KUIFAHAMU TAKUKURU na pia kujadili MAENEO YA USHIRIKIANO KATI YA TAKUKURU NA TAHLISO.