Mafunzo ya Mapambano Dhidi ya Rushwa yamefanyika Cairo – Misri kuanzia Machi 13 hadi 15, 2023 ambapo nchi za Zambia, Senegal, Congo DRC, Congo Brazaville, Madagascar, Comoro, Seychelles pamoja na Tanzania zimeshiriki. Mada mbalimbali zikiwemo kuhusu ‘Ufuatiliaji wa Mali Zilipatikana kwa Njia ya Rushwa; Majukumu ya Mamlaka za Kupambana na Rushwa katika Uzuiaji na Udhibiti wa Rushwa; Maazimio ya Umoja wa Mataifa katika Mapambano Dhidi ya Rushwa pamoja na Mikakati ya Kitaifa ya Kuzuia Rushwa zilitolewa katika mafunzo hayo ambayo TAKUKURU iliwakilishwa na Bw. Ismail Seleman Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni na Bi. Zawadi Ngailo Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha.