Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP Salum Rashid Hamduni (wa kwanza kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar – ZAECA Bw. Ali Abdalla Ali (wa pili kulia), wamekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Ushauri ya Umoja wa Afrika ya Kupinga Rushwa (African Union Advisory Board Against Corruption – AUABC) Bibi Charity H. Nchimunya (wa kwanza kushoto) – Makao Makuu ya AUABC mkoani Arusha. Mazungumzo hayo yalilenga kujadili namna ya kuandaa kwa pamoja, maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Afrika yanayotarajiwa kufanyika Julai 11, 2023 ikiwa pia ni maadhimisho ya miaka 20 ya Mkataba wa Umoja wa Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa. Viongozi wengine waliojumuika katika mazungumzo hayo ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi Neema Mwakalyelye, Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma TAKUKURU Mha. Joseph Mwaiswelo pamoja na Mkurugenzi wa Uchunguzi ZAECA Bw. Nassir Ally. TAKUKURU, ARUSHA Machi 13, 2023.