Mhe. Jenista Joakim Mhagama Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (Wa tatu kutoka
kulia) amewataka TAKUKURU kujikita zaidi katika Kuzuia vitendo vya rushwa na kutekeleza vema Programu ya TAKUKURU RAFIKI kwa lengo la
kuboresha huduma kwa wananchi. Pichani ni Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama, kulia kwake akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe. Rachel
Kassanda pamoja na Watumishi wa TAKUKURU Wilaya ya Magu wakati Waziri alipokuwa wilayani humo kwenye ukaguzi wa miradi ya TASAF. TAKUKURU
Mwanza, Februari 22, 2023.