Wajumbe wa Tume iliyoundwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa lengo la kupokea maoni ya kuboresha utendaji wa Taasisi za Haki Jinai nchini imefika na kuzungumza na Wakuu wa TAASISI za Haki
Jinai Wilayani Arumeru, Maaskari na Wananchi wa Kijiji cha Ngarasero, USA RIVER. Mwenyekiti wa Tume, JAJI Mstaafu Othman Chande (wa tatu
kutoka kushoto) aliwataka wananchi na Viongozi wa Taasisi za Haki Jinai, kuelezea kwa uhuru na bila kificho, CHANGAMOTO zozote wanazoziona wakati
wa kutoa au kupata haki kwenye vyombo vya dola. Akifafanua, maana ya HAKI JINAI, alieleza ya kwamba, “Mnyororo wa haki huanzia wakati uhalifu
unafanyika, ukamataji, upelelezi, kufikishwa mahakamani, kutolewa kwa hukumu, kufungwa gerezeni na kutoka gerezani hadi muda wa kurejea kwenye
jamii” Mkuu wa TAKUKURU (W) Arumeru Bw Deogratius Mtui ni miingoni mwa waliotoa maoni Yao. TAKUKURU ARUMERU Machi 3, 2023.