Machi 6, 2023, katika Mahakama ya Wilaya Mbeya, kumetolewa hukumu katika mashauri mawili kama ifuatavyo;- 1. Shauri la Uhujumu Uchumi Na. 15/2022 dhidi ya Suli Mwangwale na wenzake 2. Mshtakiwa wa kwanza Bw. Suli Mwangwale alikuwa Wakala wa Pembejeo za Kilimo.
Mshtakiwa wa pili Bw. Fred Mpamba alikuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mwampalala na
Mshtakiwa wa tatu Bw. Peuson Ndisa alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Pembejeo Kijiji cha Mwampalala.
Washtakiwa wote watatu walikuwa wanashtakiwa kwa makosa ya kuwasilisha nyaraka za uongo kwa Mwajiri wao na kosa la Kughushi vocha za pembejeo za kilimo.
Mahakama iliwatia hatiani kwa makosa yote na kuwapa adhabu kila mmoja kulipa faini ya shs 400,000/= au kwenda jela miaka 2.
Washtakiwa walilipa fine jumla ya shs 1,200,000/=.
- Shauri la Uhujumu Uchumi Na. 04/2022 dhidi ya Mshtakiwa Upendo Kagali.
Mshtakiwa alikuwa Afisa Mtendaji wa Kata (WEO) ya Maendeleo iliyopo Halmashauri ya (w) Mbeya.
Mshtakiwa alikuwa anashtakiwa kwa kosa la Ubadhilifu na ufujaji wa shs 2,949,500/= Mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Mahakama ilimtia hatiani na kumpa adhabu ya kulipa faini ya shs 50,000/= au kwenda jela miaka 2. Pia Mahakama ilitoa amri kuwa mshtakiwa arejeshe kiasi chote cha fedha shs 2,949,500/= alichokifanyia ubadhilifu Serikalini.