Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi. Neema Mwakalyelye, anamwakilisha Mkurugenzi Mkuu katika mkutano tajwa unaofanyika Bamako
nchini Mali. Mkutano huu unajumuisha viongozi wa juu wa Mamlaka za Kupambana na Rushwa kutoka takriban nchi 20 Barani Afrika pamoja na
wataalam mbalimbali wa Umoja wa Mataifa, ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo katika mapambano dhidi ya Rushwa. Katika
picha (katikati) ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi Neema Mwakalyelye akiongoza kikao kazi kilichojadili kuhusu ‘ Specific
Investigations on Corruption: What methodology to Adopt’. Kikao hiki kilichofanyika Februari 21, 2022 ni miongoni mwa vikao vidogo
vilivyoandaliwa kufanyika katika mkutano huo.