Mkurugenzi Msaidizi – Uchapishaji na Huduma za Maktaba katika Kurugenzi ya Elimu kwa Umma Bw. John Kabale ameshiriki mkutano huu uliofanyika kuanzia Februari 6 hadi 7, 2023 Johannesburg, Afrika Kusini.
Mkutano huu umefanyika kwa lengo la kufanya majaribio ya Miongozo ya uelewa wa jinsi ya kuzuia na kupambana na rushwa utakaotumiwa na Waheshimiwa Wabunge pamoja na wadau wengine wa nchi za Ukanda wa SADC. Vilevile mkutano huo ulijadili masuala ya Haki za Binadamu na Uimarishaji wa Utawala Bora.