Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Palestina nchini, Mheshimiwa Balozi Hamado Mansour Abu Ali, Ijumaa Februari 3, 2023. Mheshimiwa Balozi amefika TAKUKURU kwa lengo la kujadili kwa pamoja mwendelezo wa ushirikiano kati ya TAKUKURU na Mamlaka ya Kupambana na Rushwa ya Palestina ambayo tumekuwa tukishirikiana nayo.