“Kuzuia zaidi vitendo vya rushwa ndiyo dira ya Serikali ya Awamu ya Sita hivyo tunawaomba Wajumbe wa KU kushirikiana nasi katika kudhibiti rushwa. Mhakikishe usalama wa mkoa uwe ni pamoja na usalama wa fedha zinazoletwa na Serikali. Tuitumie TAKUKURU kuhakikisha azma ya Serikali inatimia”. Hayo ni maelezo aliyotoa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi. Neema Mwakalyelye Januari 19, 2023 wakati akizungumza na Wajumbe wa KU Tabora baada ya kumtembelea Mkuu wa Mkoa wa Tabora ofisini kwake. Januari 19, 2023, Tabora.