Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara Tanzania (Tanzania National Board of Commerce- TNBC) Dkt. Godwill G. Wanga – Januari 25, 2023. Mazungumzo hayo yalilenga kujadili namna ya kuzuia vitendo vya rushwa ili visiathiri mazingira ya biashara na uchumi hapa nchini. Vilevile, viongozi hao wamejadili namna ya kuwajengea uwezo Wafanyabiashara na Wawekezaji nchini ili kutojihusisha na vitendo vya rushwa. Katika hatua nyingine, Wakuu hao wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa TNBC kwa jitihada mahsusi anazozifanya katika kuzuia RUSHWA nchini.