Katika kikao kilichofanyika Januari 18, 2023, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi Neema Mwakalyelye (aliyesimama mbele katikati), amewataka watumishi hao kutekeleza majukumu kwa kuzingatia Mpango Mkakati mpya wa TAKUKURU wa Mwaka 2022/23- 2025/26. Aidha, amewataka waendelee kutekeleza majukumu yao kwa kujikita zaidi katika kuzuia vitendo vya rushwa ili kuendana na na mwelekeo wa Serikali. Vilevile, amewataka watumishi kujitahidi kuuelewa Mwongozo wa Programu ya TAKUKURU RAFIKI na kuumiliki ili kuwa mstari wa mbele katika kuitangaza programu hiyo kwa wadau mbalimbali. Vilevile, kwa kipekee zaidi amewataka watumishi hao kuwa waadilifu na kutekeleza majukumu ya Taasisi kwa weledi kwa maana kila mtumishi anayo dhamana ya kuhakikisha analeta mabadiliko katika eneo alilopo na hatimaye kuweza kufikia lengo kuu la kuwa na ” A Corruption free Tanzania”.