Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga, Januari 16, 2023, Jamhuri imeshida kesi ya Jinai yenye namba CC 56/2021 iliyokuwa ikiendeshwa na Mwendesha Mashtaka Joseph Mulebya pamoja na Khadija Luwongo kutoka TAKUKURU.
Katika kesi hii mshtakiwa alikuwa Bw. Hilton Njau aliyekuwa mtumishi wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga ambaye amekutwa na hatia ya makosa mawili ya kuomba na kupokea rushwa ya Dola za Marekani 2500, kutoka Kwa mfanyabiashara mwenye asili ya kihindi, ili asimchukulie hatua kwenye masuala ya ukwepaji kodi yaliyokuwa yakifanyiwa kazi na mshtakiwa akiwa kama Afisa Uchunguzi wa Taasisi hiyo.
Mshtakiwa ameamriwa kulipa faini ya shilingi 500,000/= kwa kila kosa ambapo kwa makosa mawili ametakiwa kulipa jumla ya shilingi 1,000,000/=. Mshtakiwa amelipa faini.