Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma limefunguliwa Shauri la Uhujumu Uchumi namba 1/2023 mbele ya Mheshimiwa Janeth Musaroche.
Jumla ya washtakiwa 6 kati ya 7 walikuwepo ambao ni:
John Bahemu- Mkurugenzi Mtendaji wa M/S Jorogi Contractors Co. LTD; na wafuatao ambao walikuwa ni wajumbe wa Timu ya Tathmini ya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwenye zabuni ya matengenezo ya miundombinu ya maji Kijiji cha Manzase-Chamwino:
- Heri Mwafute,
- George Mwakamele,
- Selemani Msafiri,
- Shaban Mpwepwe na 6. Noeli Lukuwi.
Mshtakiwa Grace Mukulusi ambaye alikuwa Mhandisi wa Maji wa H/W Chamwino alisomewa mashtaka bila kuwepo mahakamani.
Wamesomewa na kukana jumla ya mashtaka kumi, yakiwemo matumizi mabaya ya mamlaka, kujipatia manufaa na matumizi ya nyaraka kumdanganya mwajiri kinyume na PCCA; kutoa taarifa za uongo kinyume na Penal Code; na kusababisha hasara ya shilingi 264,576,174/= kinyume na EOCCA.
Wote wako nje kwa dhamana.