Januari 13, 2023 imefunguliwa Kesi ya Uhujumu Uchumi ECO. NO. 1/2023 Katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kahama Mhe. Edmund Kente.
Washitakiwa ni Bw. MICHAEL AUGUSTINO MATOMOLA, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Iramba na wenzake sita.
Kesi hiyo inaendeshwa na Waendesha Mashtaka wa TAKUKURU, SIMON MASHINGIA na JANE MBUGE, ambao waliwasomea hoja za awali za mashtaka ya kuisababishia hasara Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu ya kiasi cha sh. 138,276,250/- katika ya kipindi cha mwaka 2019.
Makosa haya yanadaiwa kutendeka wakati washtakiwa walipokuwa watumishi wa Halmashauri ya Ushetu.
Washtakiwa wamekana mashitaka na wameshindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo wamepelekwa mahabusu.
Kesi imeahirishwa hadi Januari 17, 2023 itakapokuja kwa ajili ya kusoma hoja za awali.