Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama, amezindua Program ya TAKUKURU RAFIKI inayolenga kuwashirikisha wadau katika kuzuia rushwa nchini. Uzinduzi huo umefanyika Disemba 20, 2022 sambamba na ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Viongozi wa TAKUKURU kwa Mwaka 2022. Mkutano huu umejumuisha Viongozi wa TAKUKURU 178 kuanzia ngazi ya Wakurugenzi, Wakuu wa TAKUKURU Mikoa 28 pamoja na Wakuu wa TAKUKURU Wilaya na Vituo Maalum 118.
