Viongozi ma Watumishi wa TAKUKURU mikoa ya Kilimanjaro na Arusha, wameshiriki katika kupanda Mlima Kilimanjaro katika siku ya kutimiza miaka 61 ya UHURU wa Tanzania Bara – Disemba 9, 2022.Ushiriki wa TAKUKURU unalenga kuihamasisha jamii kushirikiana na Serikali katika kuzuia rushwa nchini kwa kueneza KAULI MBIU YA TAKUKURU inayosema: KUZUIA RUSHWA NI JUKUMU LAKO NA LANGU; TUTIMIZE WAJIBU WETU.