Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni, amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Asasi ya Kiraia ya ‘ANTI CORRUPTION VOICES FOUNDATION’ – TAKUKURU Makao Makuu Dodoma. Mazungumzo hayo yalilenga kuitambua Asasi hiyo na kupongeza jitihada wanazozifanya za kushirikiana na Serikali katika KUZUIA RUSHWA kupitia Kampeni yao iitwayo: BADILI TABIA; SEPESHA RUSHWA. Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Anti Corruption Voices Foundation Bw. Dominick Kubenga (kulia kwa Mkurugenzi Mkuu) amesema, wao ni zao linalotokana na Klabu za Wapinga Rushwa zilizoanzishwa na TAKUKURU mashuleni na vyuoni, ambako wao walikuwa wanachama. Amesema Asasi yao itaendelea kueneza elimu dhidi ya rushwa kwani wanatambua kuwa jukumu la kuzuia RUSHWA ni la kila Mtanzania. Katika hatua nyingine, Anti Corruption Voices Foundation wamemkabidhi Mkurugenzi Mkuu fulana kwa ajili ya kushiriki katika mbio za ‘SEPESHA RUSHWA MARATHON’ zitakazofanyika jijini Dodoma Disemba 11, 2022.