“…Jukumu kubwa la Serikali ni kuwaletea wananchi maendeleo, hivyo usimamizi wa maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, uwazi na mapambano dhidi ya rushwa ni suala endelevu kwa kuwa ni msingi wa utoaji wa huduma bora kwa umma…” Hayo yamesemwa na Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Katiba na Sheria (katikati) wakati akizindua maadhimisho hayo ambayo yanaanza na wiki ya kutoa huduma kwa umma. Disemba 6, 2022.