Bibi. Neema Mwakalyelye Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU amekabidhiwa cheti cha shukrani na Brigedia Jenerali S.J Mkande, ambaye ni Mkufunzi Mwandamizi katika chuo cha National Defence College (NDC), kwa kutambua mchango wake wakati alipokuwa akihudumu chuoni hapo. Cheti hicho kimekabidhiwa Oktoba 26, 2022. Hatua hii imefanyika wakati Bibi. Mwakalyelye alipoenda kutoa mafunzo kwa washiriki wanaoendelea na mafunzo NDC kwa mwaka 2022.