Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini TAKUKURU, Bi. Joyce Shirima, amehitimisha mafunzo ya siku tano ya USIMAMIZI WA RASILIMAli ZA UMMA KWA MAAFISA WA TAKUKURU leo Oktoba 21, 2022.
Katika hotuba yake, Mkurugenzi huyo alisisitiza washiriki kuzingatia kilichofundishwa na kwenda kuwaelimisha wengine ili kuimarisha ufuatiliaji wa matumizi ya fedha zinazotengwa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo nchini na kuchukua hatua mapema za kuzuia ubadhirifu kama ambavyo tumekuwa tukisisitizwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mafunzo haya yamehudhuriwa na washiriki 20 kutoka mikoa ya Mwanza, Arusha, Dar es Salaam, Mbeya pamoja na Dodoma.