Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu TAKUKURU Bw. Ayoub Akida (katikati), amepokea ugeni wa Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwl. Julius Nyerere, Prof. Marcelina Chijoriga (aliyeketi kulia), aliyetembelea ofisi za TAKUKURU Makao Makuu Dodoma Oktoba 20, 2022.
Katika mazungumzo yake, Prof. Chijoriga amesisitiza umuhimu wa kuendeleza mahusiano na ushirikiano kati ya taasisi za Serikali na Shule ya Uongozi, ili kufanikisha dhamira ya maendeleo ya watumishi kama inavyosisitizwa mara kwa mara na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aliyeketi kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi- Rasilimali Watu TAKUKURU Bw. Richard Kiula.