Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi. Neema Mwakalyelye, akiwa mkoani Singida kikazi, ametembelea Wilaya ya Ikungi mkoani humo na kufuatilia utekelezaji wa Mradi wa Maendeleo ya Ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA, kilichopo wilayani Ikungi. Pamoja na mambo mengine, Naibu Mkurugenzi Mkuu alipata fursa ya kutembelea Majengo 17 ambayo yalikuwa na changamoto mbalimbali za utekelezaji lakini TAKUKURU Wilaya ya Ikungi ilipoingilia kati, mradi huo umeonesha mafanikio na thamani ya fedha zilizotumika imeonekana. Chuo hicho kwa sasa kimeshakamilika na kinatarajiwa kupokea wanafunzi kuanzia Januari 2023. Naibu Mkurugenzi Mkuu ameipongeza Kamati ya Usalama ya Ikungi kwa ushirikiano wao kwa TAKUKURU jambo ambalo lilielezwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry Muro kwamba umepelekea Wilaya ya Ikungi kutekeleza miradi yake kwa ufanisi mkubwa.