Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi. Neema Mwakalyelye amewatembelea Watumishi Wastaafu walioko katika Mkoa wa Singida, alipokuwa mkoani humo katika ziara ya kikazi, Oktoba 19, 2022. Pichani wa kwanza kushoto ni Mstaafu Bw. Coronius Mtinangi na picha ya ndani wa kwanza kulia ni Mstaafu Bw. Jafari Uledi. Wastaafu hao wamefarijika kwa kitendo cha Naibu Mkurugenzi Mkuu kuwatembelea na wameomba utaratibu huo uendelee maeneo yote kwani unaimarisha uhusiano mwema kati ya TAKUKURU na Wastaafu wake.