Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni, yuko nchini Rwanda kwa Ziara ya Mafunzo ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya KUZUIA RUSHWA. Katika ziara hiyo iliyoanza Oktoba 16, 2022, Mkurugenzi Mkuu ameongozana na Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa Bi. Sabina Seja pamoja na Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma Bw. Joseph Mwaiswelo. Hapa ni viongozi hao wakiwa katika ofisi za OMBUDSMAN zinazohusika na mapambano dhidi ya Rushwa nchini humo. Pichani juu kulia ni Mkurugenzi Mkuu akikabidhi ‘souvenirs’ kwa Chief Ombudsman Ms. Madeleine Nirere, alipotembelea ofisi za Ombudsman Oktoba 18, 2022