
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Peter Serukamba amekutana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi. Neema Mwakalyelye na kujadili mambo kadhaa yakiwemo yanayohusu kuzuia vitendo vya Rushwa katika miradi ya maendeleo na shughuli za kijamii.
Akiwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa, Naibu Mkurugenzi Mkuu amesema pamoja na mambo mengine, lengo la ziara yake ni kutembelea Mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA ulioko Wilaya Ikungi.
‘Ki msingi hapa tunatekeleza agizo la Mhe. Rais linalotutaka tujikite zaidi katika Kuzuia upotevu na ufujaji wa fedha kabla fedha haijapotea. Kama tukiweza kuyaepuka hayo tija itakuwa kubwa.” Amesema Mwakalyelye.

Aidha, amesema TAKUKURU imeendelea kujikita katika uzuiaji wa rushwa za aina zote kwa lengo la kuondoa ubadhirifu na upotevu wa fedha za Serikali.