Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni,amewataka wadau kutoka Serikalini, Taasisi binafsi pamoja na asasi za kiraia, kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni na mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007 inayotumika sasa, ili kuwa na Sheria inayoendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia pamoja na kuendelea kuijengea uwezo TAKUKURU. CP.Hamduni ameyasema hayo Septemba 22, 2022 alipokuwa akifungua warsha ya siku mbili ya wadau ya kujadili na kutoa maoni na mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na. 11 ya mwaka 2007 inayofanyika jijini Dodoma.